Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 10:46

Assad akanusha kutumia silaha za kemikali lakini akubali kuzisalimisha


Rais wa Syria, Bashar Al-Assad (kulia) na naibu waziri wa mambo ya nje wa Russia, Sergei Ryabkov huko Damascus, Septemba 18,2013
Rais wa Syria, Bashar Al-Assad (kulia) na naibu waziri wa mambo ya nje wa Russia, Sergei Ryabkov huko Damascus, Septemba 18,2013
Rais wa Syria Bashar al-Assad anasema anania ya dhati ya kuteketeza silaha za kemikali kwenye ghala lake lakini anakanusha majeshi yake yalifanya shambulizi la gesi ya sumu mwezi uliopita ambalo liliuwa mamia ya wananchi karibu na Damascus.

Katika mahojiano na kituo cha televisheni cha Fox News cha Marekani, Assad aliahidi kusubiri mpango wa Marekani na Russia unaolenga kutokomeza maghala ya silaha lakini alielezea hali kuwa ni ya utatanishi akisema kuteketeza silaha kutagharimu kiasi cha dola bilioni moja na itachukua mwaka mmoja au pengine zaidi ya hapo.

Mpango wa kuteketeza ambao bado unajadiliwa na wawakilishi wa baraza la usalama la Umoja wa mataifa unaitaka serikali ya Syria kuwasilisha maelezo ya kina ya silaha zake za kemikali ifikapo Jumamosi. Assad alisema yupo tayari kufanya hili kwa maneno yake hata “kesho” na anaweza kutoa njia kwa wataalamu kuelekea kwenye vituo ambako silaha zinahifadhiwa.

Wakati huo huo, kiongozi huyo wa Syria aliikosoa ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa wiki hii ambayo inathibitisha gesi aina ya SARIN ilitumika katika shambulizi dhidi ya raia katika kiunga kilichoshikiliwa na waasi cha Ghouta hapo Agosti 21. Japokuwa ripoti haikuelezea malalamiko, mataifa ya Marekani na magharibi yalisema yanaunga mkono wa dhati kwamba majeshi ya serikali na sio ya waasi yalihusika kwa shambulizi la Agosti 21.
XS
SM
MD
LG