Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 14:06

Hosni Mubarak augua saratani ya tumbo


Picha ya waandamanaji wanaoipinga serikali ya Misri wakifurahia kuondoka kwa rais wa zamani Hosni Mubarak
Picha ya waandamanaji wanaoipinga serikali ya Misri wakifurahia kuondoka kwa rais wa zamani Hosni Mubarak

Wakili wake Farid el- Deeb alisema jumatatu kwamba rais huyo aliyetimuliwa madarakani amefanyiwa upasuaji mkubwa huko Ujerumani


Wakili wa rais wa zamani wa Misri Hosni Mubarak amesema kiongozi huyo aliyelazwa hospitali anasumbuliwa na saratani ya tumbo.

Farid el- Deeb alisema jumatatu kwamba rais huyo aliyetimuliwa madarakani mwenye umri wa miaka 83 amefanyiwa upasuaji mkubwa huko Ujerumani mwaka jana kuondolewa sehemu iliyokuwa imeathiriwa na saratani na sehemu ya kongosho.

Amesema kuna ushahidi kwamba saratani hiyo imerejea tena. Wakili huyo amesema bwana Mubarak amekuwa akiahirisha kufanyiwa uchunguzi wa mara kwa mara wa afya yake huko Ujerumani uliotakiwa kufanyika kila baada ya miezi minne.

Lakini shirika la habari la Associated Press lilimnukulu mkuu wa maswala ya afya wa rais huyo wa zamani Assem Azzam, akikanusha ripoti kuwa Bwana Mubarak ana saratani na kuielezea hali yake kuwa thabiti.

Shirika hilo linanukulu pia afisa wa afya katika hospitali ya Sharm el-Sheikh ambako Bwana Mubarak amelazwa tangu Aprili 13 akisema kuwa rais huyo ana tatizo la moyo na kwamba hajalazwa katika chumba cha wagonjwa mahtuti.

XS
SM
MD
LG