Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 07:30

Viongozi wa Amerika Kaskazini wapinga kutokuunga mkono utandawazi


Rais wa Mexico Enrique Pena Nieto (kushoto), Waziri mkuu wa Canada Justin Trudeau na rais wa Marekani Barack Obama
Rais wa Mexico Enrique Pena Nieto (kushoto), Waziri mkuu wa Canada Justin Trudeau na rais wa Marekani Barack Obama

Viongozi wa Marekani ,Canada na Mexico wamekataa kwa kiasi kikubwa mpango wa kulinda biashara na kutokuunga mkono utandawazi jumatano katika mkutano wa viongozi wa Amerika kaskazini.

Rais wa Marekani Barack Obama , waziri mkuu wa Canada Justin Trudeau na rais wa Mexico Enrique Penya Nieto walisifu faida za mkataba wa biashara huru wa Amerika kaskazini (NAFTA) uliodumu kwa miaka 22 katika wakati ambapo biashara za kimataifa zinashambuliwa Marekani na Ulaya . Kwa pamoja nchi hizo tatu zinajumuisha asilimia zipatazo 27 ya uchumi duniani.

Waziri mkuu wa Canada Justin Trudeau alisema mkutano huo ulikuwa wa huzuni kidogo kwasababu ya kile alichokiita matarajio ya kustaafu rais Obama. Watatu hao walieleza urafiki wao wa karibu na jinsi wanavyoheshimiana na kusisitiza neno la “3 amigos” –ikimaanisaha marafiki watatu jina la utani ambalo vyombo vya habari vimewapa.

Obama Trudeau na Pena Nieto walikubaliana kuunga mkono uzalishaji wa nishati safi kwa Amerika kaskazini katika miaka 10 ijayo wakilenga kuzalisha nusu ya umeme wa Amerika Kaskazini kutoka kwenye vyanzo visivyokuwa Carbon ifikapo 2025.

XS
SM
MD
LG