Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 19:12

Al-Shabaab yauwa maafisa 5 wa polisi Mandera, Kenya


Kundi la kigaidi la Al-Shabaab nchini Somalia
Kundi la kigaidi la Al-Shabaab nchini Somalia

Ofisa mmoja wa mji wa Elwak, kaskazini mashariki ya Kenya, amesema maafisa watano wa Polisi wameuwawa baada ya wanamgambo wanaoshukiwa ni wa al-Shabaab kushambulia msafara wa magari ya polisi wakati ulipokua unasafiri kwenye eneo la kaskazini-mashariki mwa nchi hiyo.

Polisi hao walikuwa wakishindikiza basi moja kutoka Mandera kuelekea Nairobi wakati wanamgambo walipolipua gari lao karibu na Elwak. kwa kile kinachoaminika kuwa guruneti iliyofyatuliwa kwa roketi.

Gavana wa kaunti ya Mandera, Ali Rioba alisema kwenye ukurasa wake wa twitter kwamba “tunalaani shambulizi lililofanywa na al-Shabaab huko Dimu asubuhi hii, na maafisa watano wameuliwa.”

Msemaji wa kundi la al-Shabab amelieleza shirika la habari la Reuters kwamba wanamgambo wao walihusika na shambulizi hilo.

Kundi la Al-Shabaab lenye uhusiano na al-Qaida huko Afrika mashariki lenye makao yake nchini Somalia mara kwa mara hufanya mashambulizi nchini kenya. Mpaka wa Kenya na Somalia unaonekana kama kituo dhaifu kwa usalama kutokana na kwamba ni eneo la mbali na kukosekana kwa ushirikiano kati ya polisi kutoka pande zote.

XS
SM
MD
LG