Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 14:55

Al-Shabab washambulia jengo la serikali ya Somalia


Wanamgambo wa kundi la al-Shabab la nchini Somalia
Wanamgambo wa kundi la al-Shabab la nchini Somalia

Wanamgambo wa al-Shabab washambulia jengo moja la serikali na kusababisha vifo vya watu kadhaa

Kundi la wanamgambo wa ki-Islam la al-Shabab linasema limefanya shambulizi moja lililosababisha mauaji katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu, Jumatano.

Tume ya Umoja wa Afrika-AU nchini Somalia inasema mlipuko wa bomu uliotokea nje ya jengo moja la serikali uliuwa watu wasiopungua watatu.

Msemaji wa AU anasema mlipuko ulitokea nje ya jengo moja linalotumiwa na spika wa bunge, Sharif Hassan Sheikh Aden. Haikufahamika mara moja kama spika huyo alikuwa mlengwa.

Serikali ya Somalia inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa iliyaondoa majeshi ya al-Shabab katika mji wa Mogadishu mwaka jana, lakini kundi hilo lenye uhusiano na al-Qaida linaapa kuendeleza mashambulizi. Al-Shabab inaendelea kudhibiti sehemu za kusini na kati kati ya Somalia.

Somalia haijakuwa na serikali thabiti tangu mwaka 1991. Nchi hiyo pia inajaribu kuondokana na ukame mbaya na njaa ambayo iliwakosesha makazi maelfu ya wasomali.

XS
SM
MD
LG