Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 18:36

Air Zimbabwe yasitisha safari zake za nje


Ndege ya shirika la ndege la Air Zimbabwe
Ndege ya shirika la ndege la Air Zimbabwe

Shirika la ndege la taifa la Zimbabwe, Air Zimbabwe limesitisha safari zake zote za kikanda baada ya kampuni moja ya kutoa mkopo kuchukua ndege iliyokuwa imelikopesha shirika hilo kwa sababu ya kutolipa deni lake.
Hatua hiyo ni pigo jingine kubwa kwa shirika hilo la taifa lenya kukabiliwa na matatizo ya kifedha.

Chama cha kimataifa cha usafiri wa ndege kilisimamisha uwanachama wa Zimbabwe kuweza kutumia idara za kupanga safari za ndege kuanzia siku ya Jumapili, kwa sababu ya kutolipa ada ya dola 280,000.

Matatizo hayo yaliongezeka Jumanne wakati shirika la ndege la Zambezi Airlines leneye makao yake Zambia lilipochukua ndege tena yake ya aina ya Boeing 737 iliyokuwa imekodishwa Air Zimbabwe kwa sababu ya kutolipwa deni la dola 460,000.

Air Zimbabwe iliikodisha ndege hiyo ili kuchukua nafasi ya ndege zake za zamani zilizositishwa kufanya kazi mwezi uliopita.

Matatizo ya shirika hilo la ndege yamekuwa yakiongezeka kwa utaratibu mnamo miaka ya hivi karibuni kwa sababu ya uongozi mbaya na kuzeeka kwa ndege hizo. Wakosoaji wanasema kushindwa kutatua matatizo hayo kumechangia washindani wengine kuchukua njia za safari za Air Zimbabwe.

XS
SM
MD
LG