Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 07:11

Umoja wa Mataifa waahidi kuteketeza baa la njaa duniani


Umoja wa mataifa umefungua mkutano wa siku tatu wa usalama wa chakula, ukiapa kuchukua hatua kuteketeza baa la njaa duniani lililoathiri watu bilioni moja kote duniani.

Hata hivyo wajumbe katika mkutano huko Rome walishindwa kufikia ahadi ya dola bilioni 44 za msaada ulioombwa na shirika la chakula la umoja wa mataifa na kilimo na azimio la mwisho katika mkutano huo uliofanyika Novemba 16 halikuwa na ahadi zozote mpya za kifedha.

Wachambuzi wanasema azimio hilo pia halikusema lolote kuhusu lengo la Umoja wa mataifa kuteketeza njaa duniani ifikapo mwaka 2025. Katika hotuba yake ya ufunguzi katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki Moon aliwaambia wakuu wa nchi na serikali hakutaweza kuwa na usalama wa chakula bila kuwepo usalama wa hali ya hewa.

Wakati huo, huo nchini Tanzania, mikoa 16 imeathiriwa mno na njaa, kufuatia ukame wa muda mrefu. Mkurugenzi wa kitengo cha maafa , kinachoshughulikia maswala ya usalama wa chakula, bwana Joseph Shiyo aliiambia sauti ya Amerika katika mahojiano kuwa serikali tayari imeanza kugawa chakula kwa watu walioathirika zaidi katika mikoa hiyo.

XS
SM
MD
LG