Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 18:32

Clinton awataka wacongo kujiamini


Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Hillary Clinton amewasili Kinshasa na alitembelea hospitali iliyojengwa na mcheza mpira wa kikapu wa zamani Dikembe Mutombo na pia kukutana na wanafunzi wa vyuo vikuu vya huko. Mwandishi wetu Salehe Mwanamilongo ametuletea ripoti kuwa Bi Clinton alistushwa na ubora wa hospitali hiyo ya kisasa na kusema kwamba ikiwa wacongo watachukua dhamana yao wenyewe kufanya vitu kama hivyo watasaidia kuchangia maendeleo ya nchi yao na Dikembe Mutombo ni mfano mzuri. Aidha amewataka wananchi wa Congo kusahau yaliyopita na kujenga nchi yao wakati alipozungumza na wanafunzi wa vyuo vikuu. Anatagemewa kukutana na Waziri Mkuu jioni ya Jumatatu, wafanya biashara na viongozi wa mashirika ya kutetea haki za binadamu. Ziara yake ni ya saa 48 na hapo kesho atakutana na wanawake waliobakwa na pia Rais Joseph Kabila kuzungumzia uhusiano wa nchi hizo mbili.

XS
SM
MD
LG