Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 13:12

Viongozi waahidi kuimarisha usalama wa nuklia


Viongozi waahidi kuimarisha usalama wa nuklia
Viongozi waahidi kuimarisha usalama wa nuklia

<!-- IMAGE -->

Rais Barack Obama amesema kwamba mkutano wa mataifa 47 juu ya usalama wa nuklia, ulomalizika Jumanne mjini Washington, ni hatua muhimu kufikia lengo la kulinda zana za nuklia katika muda wa miaka minne ijayo.

Taarifa ya mwisho ya mkutano huo wa siku mbili unataja hatua ambazo kila nchi imesema itachuku, ingawa kwa hiyari, katika lengo la kupunguza uwezekano wa makundi ya kigaidi kupata zana za nuklia.

Taarifa hiyo yenye ukurasa tatu, inawataka viongozi waloshiriki kuhakikisha wamehifadhi kwa usalama zana zao zote za nuklia ifikapo 2014 na imeorodhesha masahrti 12 maalum lazima yatekelezwe ikiwa ni pamoja na ahadi ya kuhakikisha zana za nuklia katika nchi zao zinalindwa kwa usalama wa kutosha.

Mataifa yameahidi miongoni mwa mambo mengi kuyazuia makundi au mashirika yasio ya kitaifa kupata habari au teknolojia inayohitajika kutumia zana za nkulia kwa malengo ya kikatili. Pamoja na kutambua haja ya ushirikiano ili kuzuia kwa dhati na kukabiliana namatukiyo ya biashara haramu ya nuklia.

XS
SM
MD
LG