Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 15:50

Majeshi ya DRC yachukua tena udhibiti Mbandake


Majeshi ya DRC yachukua tena udhibiti Mbandake
Majeshi ya DRC yachukua tena udhibiti Mbandake

<!-- IMAGE -->

Majeshi ya serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo yamechukua tena udhibiti wa uwanja wa ndege wa mji mkuu wa jimbo la Equateur, Mbandaka. Redio inayoendeshwa na Umoja wa Mataifa nchini humo, Radio Okapi imeripoti kwamba, baada ya mapigano makali majeshi ya serekali yakisaidiwa na majeshi ya kulinda amani MONUC yamechukua tena udhibiti wa uwanja wa ndege.

Siku ya Jumapili, wapiganaji wasiopungua 30 kutoka kabila la Enyele waliwashambulia wanajeshi wa serekali na walinda amani huko Mbandaka. Msemaji wa MONUC, Madnoudje Mounoubai amesema, waasi waliwasili kwa boti kupitia mto Kongo na kushambulia kwanza makazi ya gavana kabla ya kuushambulia uwanja wa ndege.

Msemaji huyo alisema mlinda amani mmoja kutoka Ghana aliuliwa kwa bahati mbaya kutokana na risasi ambayo haikulengwa dhidi yake. Jeshi la Kongo lilikua limepeleka wanajeshi zaidi mwishoni mwa mwaka jana huko Equateur kujaribu kuzuia mapambano kati ya makabila ya Enyele na Monzaya.

Makabila hayo mawili wanapigania haki za kulima na uvuvi katika eneo la Dongo. Mashirika ya huduma za dharura yanasema mapigano hayo yalisababisha vifo vya watu 100, na karibu watu laki mbili wamepoteza makazi yao.

XS
SM
MD
LG