Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 01:09

Clinton Aendelea na ziara Amerika Kusini


Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Hillary Clinton yuko Brasilia kwa ajili ya mikutano na maafisa wa Brazil baada ya kusimama Chile ambako aliahidi msaada wa muda mrefu kutoka Marekani kusaidia nchi hiyo iliyokumbwa na tetemeko la ardhi.

Maafisa wa Chile wanasema hasara inakisiwa kufikia mabillioni ya dola.

Clinton alisimama kwa saa chache tu katika uwanja wa ndege wa Santiago, ambapo alikutana na Rais Michelle Bachelet na rais-mteule Sebastian Pinera, na kutoa awamu ya kwanza ya simu za satalaiti zinazohitajika sana nchini humo.

Lakini aliahidi kuwa Marekani ina nia ya kutimiza maombi ya Chile ya orodha ya vitu vya dharura vinavyohitajika, ikiwa ni pamoja na magari ya wagonjwa yenye vifaa va kufanyia operesheni ndani yake na vifaa vya kusafishia maji, na kuahidi kuwa Marekani itaisaidia Chile kwa muda mrefu.

XS
SM
MD
LG