Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 15:18

Serikali ya Zimbabwe yateuwa wakuu wa tume


Wazimbabwe wawili wanaoheshimika nchini humo wameteuliwa kuongoza tume mbili mpya - za haki za binadamu na tume ya uchaguzi. Uteuzi huo umefanyika baada ya miezi kadha ya mashauriano magumu na kufanikiwa kwake ni dalili ya maendeleo katika siasa za mvutano nchini humo.

Sehemu muhimu ya mkataba wa Septemba 2008 uliounda serikali ya umoja wa taifa Zimbabwe mwaka mmoja uliopita ni kuteuliwa kwa kiongozi mpya wa tume ya uchaguzi na kuunda kwa tume ya haki za binadamu. Serikali sasa imeamua nani wataongoza tume hizo mbili.

Mwenyekiti mpya wa tume ya uchaguzi ni Jaji Simpson Mtambanengwe, raia wa Zimbabwe aliyekuwa akifanya kazi na mahakama za Nambia tangu 1994 ambako aliwahi kuwa Jaji Mkuu na mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Windhoek. anachukua nafasi ya George Chiweshe aliyekuwa mwenyekiti wa tume ya uchaguzi uliopita.

Professa Reg Austin atakuwa mwenyekiti wa kwanza wa Tume ya Haki za Binadamu, Zimbabwe. Alikuwa mshauri wa maswala ya sheria wa kiongozi wa zamani Joshua Nkomo wakati wa mazungumzo ya uhuru London mwaka 1979.

XS
SM
MD
LG