Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 16:44

Mapigano  mapya Somalia


Mashahidi katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu wanasema watu 8 wamekufa katika mapigano makali kati ya waasi na majeshi yanayoiunga mkono serikali.

Wakazi wanasema wanamgambo wa ki-Islam walifyatua makombora kwenye makazi ya Rais Jumapili jioni, na kuwachochea wanajeshi wa serikali au majeshi ya walinda amani wa Umoja wa Afrika kujibu shambulizi hilo kwa risasi.

Makombora mengi yalipiga kwenye nyumba huko kaskazini mwa Mogadishu. Ali Musa mkuu wa huduma za gari la wagonjwa katika mji huo anasema watu 55 walijeruhiwa na baadhi yao wako mahututi.

Rais wa Somalia Sheikh Sharif Sheikh Ahmed hakuwepo kwenye makazi hayo wakati shambulizi linatokea. Yupo Ethiopia ambako anahudhuria mkutano wa Umoja wa Afrika. Hili ni shambulizi kubwa la pili la mapigano huko Mogadishu katika muda wa siku 3. Ijumaa watu 15 waliuwawa baada ya wapiganaji kutoka kundi la uasi la al-Shabab kuvamia kituo kinachodhibitiwa na wanajeshi wa serikali na wanamgambo wa AU.

XS
SM
MD
LG