Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 17:43

Rais wa Nigeria atakiwa kukabidhi madaraka


Baraza la mawaziri la Nigeria limeamua kuwa rais wa Nigeria Umaru Yar’Adua ambaye anaumwa bado ana afya ya kuweza kuendelea kuongoza licha ya kutokuwepo nchini kwa miezi miwili.

Uamuzi wa baraza hilo umepingana na baraza la Seneti ambalo linasema rais lazima alijulishe bunge rasmi kuhusu kutokuwepo kwake - hatua itakayomaanisha hana budi kukabidhi madaraka kwa makamu wake.

Maamuzi yote yalikuja Jumatano wakati viongozi wa serikali walipokuwa wakijadiliana kama rais Yar’Adua ana uwezo wa kuendelea na shughuli zake.

Aliondoka kwenda Saudi Arabia mwishoni mwa mwezi Novemba kwa matibabu ya moyo. Kiongozi huyo pia ana matatizo ya figo.

XS
SM
MD
LG