Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 18:07

Clinton Aenda Haiti


Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton, ambae ni mjumbe maalum wa Umoja wa Matiafa kwa ajili ya Haiti alitembelea taifa hilo lililoharibika kutokana na tetemeko la ardhi.

Ziara yake inafanyika wakati wafanyakazi wa kimataifa wa kutoa huduma wakijaribu kusaidia walionusurika katika tetemeko kubwa la Jumanne iliyopita. Bw. Clinton alisema Jumapili kuwa atapeleka misaada na kukutana na Rais Rene Preval na maafisa wengine wa serikali ya Haiti.

Wakati huo huo, raia wa Haiti walifanya ibada za kidini juu ya makanisa yaliyofukiwa kwenye vifusi jumapili, huku waokoaji wakiendelea kuchimba chini ya vifusi kuwaokoa watu walionaswa,na mashirika fadhili yakiwasaidia waathiriwa wa tetemeko hilo la jumanne.

Timu ya waokoaji ya Marekani iliwaokoa watu watatu walionusurika kifo baada ya kuwakuta chini ya vifusi kwenye duka moja kubwa lililoporomoka katika mji mkuu Port–au–Prince.
Na mwanamue mmoja raia wa Denmark ambaye pia alikuwa mfanyikazi wa shirika la Umoja wa mataifa aliokolewa baada ya kufukuliwa chini ya jengo la Umoja wa mataifa lililoporomoka.

XS
SM
MD
LG