Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 03:43

Maandamano katika mkutano wa Copenhagen


Mamia ya waandamanaji walikusanyika kwenye eneo la mkutano wa hali ya hewa wa Umoja wa Mataifa huko Copenhagen, huku viongozi wa dunia wakijiandaa kukutana katika jaribio la kupata mkataba mpya wa hali ya joto joto duniani.

Wanaharakati wa hali ya hewa, waliokasirishwa na kasi ndogo ya mazungumzo, waliandamana kwenye kituo cha Bella leo Jumatano, ambapo viongozi kutoka zaidi ya nchi mia moja wanakusanyika kwenye mkutano. Polisi wanasema zaidi ya waandamanaji mia moja walikamatwa baada ya kuvunja uzio wa eneo la usalama.

Siku tisa za mazungumzo hazijazaa matunda yeyote na baadhi wanasema kwamba wajumbe wanatumia muda mwingi kuelezea na kurudia vitu hivyo hivyo badala ya kupata suluhisho.

Waziri mkuu wa Uingereza Gordon Brown, ambaye yupo Copenhagen kwenye mkutano huo alisema kushindwa kupata hatua muafaka zinaweza kuathiri kiwango cha maisha ya mamilioni ya watu.

White House inasema Rais Barack Obama ana matumaini kwamba mkataba unaweza kufikiwa wiki hii. Viongozi wa dunia wana mpaka siku ya Ijumaa kuafikiana hatua za mwisho za kupunguza utoaji wa gesi chafu au kutoa msaada kwa nchi maskini kukabiliana na athari za joto joto duniani.

XS
SM
MD
LG