Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 08:24

Wizara ya Afya Tanzania Yaelezea  H1N1


Wizara ya Afya nchini Tanzania imetoa taarifa juu ya kuibuka kwa virusi vya H1N1, vinavyosababisha ugonjwa wa homa ya mafua ya nguruwe katika maeneo mbali mbali nchini humo.

Kaimu katibu mkuu wa wizara ya afya na ustawi wa jamii nchini Tanzania, Dk Deo Mtasiwa, amewaambia waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam, siku ya Ijumaa kwamba idadi ya wagonjwa waliothibitika kuwa na homa ya mafua ya nguruwe mpaka kufikia Novemba 26 mwaka huu ni 599, ambapo kati yao 488 ni raia wa Tanzania.

Maeneo yaliyoathirika na ugonjwa huo ni mkoa wa Dar Es Salaam wagonjwa mia moja na tisini na saba, wilaya ya Mbulu wagonjwa 384, mkoa wa Mara mgonjwa mmoja, na mkoa wa Mwanza katika wilaya ya Kwimba kuna wagonjwa kumi na nne. Dk.Mtasiwa pia alisema hadi kufikia tarehe 26 mwezi huu, idadi ya wagonjwa ambao walikwenda kwenye kituo cha Kwimba ni mia moja na arobaini na mbili.

Amesema sampuli walizozipokea kuzipima ni ishirini na nne, na kati ya hizo kumi na nne zimegundulika kuwa na virusi vya ugonjwa huo na wagonjwa hao wamepewa maelekezo ya kutosha namna ambavyo watajikinga ili wasiweze kuambukiza mtu mwingine, lakini pia wananchi wa Kwimba wameelimishwa vizuri namna ya kujikinga na ugonjwa huo ili wasiweze kuambukiza kwa mtu mwingine.

Wakati huo huo wagonjwa wapatao 40 wa homa ya mafua ya nguruwe ambao walionekana hali zao hazifai kuruhusiwa kurudi nyumbani wamewekwa kwenye kituo kimoja huko Kwimba.

Zinazohusiana

XS
SM
MD
LG