Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 11:37

Jeshi la Nigeria lasema utulivu umerudi Niger Delta


Jeshi la Nigeria linasema kuwa eneo lenye utajiri wa mafuta la Niger Delta limerejea katika hali ya utulivu, baada ya miaka ya mashambulio yaloharibu miundo mbinu ya mafuta na kuleta hali ya kutokuwepo kwa usalama.
Jeshi linasema ingawa linakaribisha usitishaji mapigano, lakini mkakati wake ni kupigana dhidi ya mtandao wa magenge ya kihalifu yanohusika katika wizi wa mafuta ghafi unaendelea huko Niger Delta.

Msemaji wa jeshi la Nigeria huko Niger delta Timothy Antigha, anasema usitishaji mapigano ya miezi minne sasa, imerudisha tena hali ya uthabiti katika eneo lenya utajiri wa mafuta lililokua na matatizo la kusini mwa nchi hiyo.

Antigha anasema, “wa-Nigeria na wageni, kwa miezi mitatu hadi minne sasa, wamekuwa wakifanya shughuli zao bila ya hofu ya usalama. Kutokana na hayo kikosi maalum cha pamoja cha jeshi kimefanikiwa sana katika kuhakikisha kuwa hali ya kawaida imerudi. Na kwamba watu wanaendelea na shughuli zao bila hofu yeyote ya kutokuwepo kwa usalama.”

Hapo mwezi Juni rais Umaru Yaradua, alitowa msamaha kwa wanaharakati huko Niger Delta. Jambo hilo lilikua na lengo la kumaliza miaka ya mapigano katika eneo hilo ambalo limegharimu msafirishaji mkuu wa mafuta, barani Afrika kupoteza mabillion ya dola ya mapato.

Zaidi ya wanaharakati elfu 8 walisalimisha silaha zao na kukubali mpango wa msamaha. Ukosefu wa usalama kwa muda mrefu umeathiri vibaya biashara ya mafuta ya Nigeria, na wakazi wa jimbo hilo la Niger Delta wamekasirishwa kutokana na kuendelea kuwa katika hali ya umasikini ingawa kwa miongo mitano, mafuta yamekuwa yakizalishwa katika eneo hilo.

Wakuu wa viwanda vya mafuta wanasema hali ya usalama bado iko dhaifu, japo kua ghasia zimepunguwa. Tayari baadhi ya wanaharakati wasoridhika wamekasirika kwa kutolipwa marupurupu yao na wametishia kurudia tena kufanya ghasia iwapo hawatalipwa marupurupu yao.

Serikali ya Nigeria inasema mpango huo wa msamaha ni hatua ya kwanza ya kuleta amani kwa eneo hilo na imeweka mipango ya kuendeleza eneo la Niger Delta.

XS
SM
MD
LG