Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 09:55

Wanawake watoa wito wa mabadiliko Zanzibar


Jumuia ya wanawake wa chama cha upinzani huko Zanzibar CUF, waliandamana Unguja jana kuunga mkono uwamuzi wa viongozi wao kuitambua serekali ya Rais Amani Karume.

Akizungumza na Sauti ya Amerika kutoka Zanzibar katibu mkuu wa Jumuia ya wanawake wa CUF Zahara Hamadi alisema, mandamano yalikua maalum kwa ajili ya wanawake wa chama cha CUF na ndiyo maana hapakuwepo na idadi kubwa ya watu.

Alisema, "tunatarajia kupata Zanzibar mpya, Zanzibar ambayo itakua na neema na maendeleo, lakini vile vile tunatarajia tutapata Zanzibar yenye utulivu na amani ya kweli"

Mapema mwezi huu kiongozi wa CUF huko Zanzibar Seif Sharif Hamadi, alitangaza kumtambua rasmi Rais Amani Karume kama hatua ya kutafuta ufumbuzi wa mzozo wa kisiasa visiwani humo. Hatu hiyo imepongezwa na watu wa pande zote za kisiasa huko Zanzibar.

Bi Zahara Hamadi alisema wanawake wamefurahi na uwamuzi huo kwa sababu ni wanawake wanaoathirika zaidi kutokana na mivutano ya kisiasa na kushindwa kwa siasa za visiwani humo. Anasema kukubali kwa wanasiasa kutanzua tofauti kazi yao ni heri kwa wanawake na wananchi wote kwa ujumla.

XS
SM
MD
LG