Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 08:10

Makundi ya kutetea haki Zimbabwe yasusia mkutano wa serekali.


Vyama vya wataalam wa maswala mbalimbali nchini Zimbabwe kikiwemo kile cha mawakili wa kutetea haki za binadamu nchini humo, vimesema havitohudhuria mkutano ulioandaliwa na chama tawala cha ZANU-PF na kusimamiwa na wizara ya sheria.

Kususiwa kwa mkutano huo na vyama hivyo, kunaashiria pigo kubwa zaidi katika serikali dhaifu ya umoja wa kitaifa.

Mkutano huo uliodhaminiwa na serikali ulitazamiwa kufanyika alhamis huko Victoria Falls, na ungekuwa wa kwanza wa aina yake tangu kubuniwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa mwezi Februari. Wajumbe walitazamiwa kuzungumzia uwezo wa kupata haki za kisheria kwa wazimbabwe wote na namna mfumo wa kisheria wa Zimbabwe unavofanya kazi.

Lakini chama cha mawakili wa Zimbabwe kinasema namna kesi zinavyoendeshwa; watu kukamatwa ovyo, kuwekwa kizuzini kwa watetezi na wanaharakati wa haki za binadamu pamoja na ukiukwaji wa katiba ya Zimbabwe ni mambo yanayoendelea bila serikali kujali, na hivyo basi hawatahudhuria mkutano huo.

Mawakili hao wanasema kutokana na hali hiyo raia wengi wa Zimbabwe hawana imani na mfumo wa kisheria nchini humo.

XS
SM
MD
LG