Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 08:10

Marekani yaiwekea Sudan vikwazo


Rais wa Marekani Barack Obama ameweka upya vikwazo dhidi ya Sudan, akisema hatua za serikali ya nchi hiyo zinaendelea kuwa kitisho cha usalama kwa nchi ya Marekani.

Vikwazo hivyo vinadhibiti biashara na uwekezaji baina ya Marekani na Sudan, na pia vinalenga marufuku ya kusafiri na kuzuia mali, za baadhi ya maafisa wakuu wa Sudan.

Rais Obama alisema angeweka upya vikwazo hivyo, alipotangaza sera mpya za utawala wake kwa Sudan wiki iliyopita. Sera hizo mpya kwa Khartoum zinalenga kuishinikiza serikali hiyo kuongeza juhudi za kuleta amani, na kuionya kuwa itakabiliwa na shinikizo zaidi kutoka kwa Marekani endapo hatazingatia hilo.

Marekani inataka kuona mzozo wa Darfur umetatuliwa pamoja na utekelezaji kamili wa mkataba wa amani uliofikiwa baina ya Kaskazini na Kusini, na kuhakikisha Sudan haitakuwa maficho ya magaidi wa kimataifa.

XS
SM
MD
LG