Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 16:31

Obama apokea kwa mshangao na unyenyekevu tunzo ya amani


Rais Barack Obama amekua mshindi wa tunzo ya amani ya Nobel mwaka 2009. Mwenyekiti wa kamati ya Nobel Thorbjorn Jagland, anasema wamemteua rais Obama kwa sababu ya juhudi zake za kuimarisha uhusiano mwema kati ya watu wa dunia. Bw Jagland amesema, tangu kuchukua mnadaraka ameanzisha juhudi za kupunguza silaha za hatari hasa nuklia, na kuimarisha ushirikiano na mashirika ya kimataifa.

Akizungumza na waandishi habari kufuatia habari hizo, rais Obama alisema alishangazwa na wakati huo huo alipokea habari hizo kwa unyenyekevu kabisa kutoka kamati ya Nobel ya Norway.

Rais Obama alisema, 'hebu nifafanuwe hapa, sichukuli hii ni kutambua mafanikio yangu binafsi, bali ni kuthibitisha uwongozi wa Wamarekani kwa niaba ya matumaini waliyo na wato katika mataifa yote."

Bw Obama alichukua madaraka siku 12 kabla ya siku ya mwisho ya Febuari mosi, kuwasilisha majina ya watakaoteuliwa. Baadhi ya wafuatiliaji masuala ya Nobel wanasema amepewa tunzo hiyo mapema, ukichukulia kwamba juhudi nyingi za kidiplomasia za rais hazijaleta matunda bado.

Hata hivyo, ingawa kulikua na maoni tofauti duniani lakini viongozi wengi na watu walipongeza uwamusi huo. Abdul Nanji, mhadhiri wa chuo kikuu cha Cornell, New York ameimabia sauti ya amerika kwamba kupewa tunzo hiyo ni kutokana na mawazo yake, uwongozi wake na matumaini makubwa aliyeleta katika kubadili namna Marekani inavyo wasiliana na nchi nyengine za ulimwengu.

XS
SM
MD
LG