Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 23:57

Waathirika wa Mabomu 1998 Tanzania waandaa Kesi


Waathirika wa mabomu yaliyolipuka katika ubalozi wa Marekani nchini Tanzania mwaka 1998, wameanza kukusanya vielelezo vyao vinavyothibitisha namna walivyoathirika na mabomu hayo, kwa ajili ya kuwasilisha katika mahakama moja inayosikiliza kesi hiyo iliyopo mjini Washington ili waweze kulipwa fidia zao.

Muathirika mmoja raia wa Marekani ambaye alijeruhiwa vibaya katika tukio hilo yupo Dar-Es-Salaam nchini Tanzania ambapo anafanikisha ukusanyaji wa vielelezo hivyo na kuwasilisha mahala husika.

Milipuko ya mabomu katika ubalozi wa Marekani nchini Tanzania, ilitokea sambamba na milipuko kwenye ubalozi wa Marekani nchini Kenya ambapo mamia ya watu walipoteza maisha na kujeruhiwa vibaya na hata kusababishiwa vilema vya maisha.

Tangu wakati huo kumekuwa na mvutano namna ya kuwalipa fidia waathirika waliofikwa na mkasa huo, huku serikali ya Marekani ikisisitiza iko tayari kuwalipa watumishi wake waliokuwa ubalozini, wakati raia wengine wa kawaida wakiachwa bila mwelekeo, jambo ambalo lilipelekea raia wa kawaida kufika kwenye mfumo wa sheria, hasa mahakamani.

XS
SM
MD
LG