Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 07:49

Viongozi wa dunia waikemea Iran


Rais wa Marekani Barack Obama na viongozi wengine wa magharibi wanaishutumu Iran kwa kujenga kituo cha siri cha nyuklia, madai ambayo Iran imeyakanusha.

Bwana Obama, Waziri Mkuu wa Uingereza Gordon Brown na Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy walitoa matamshi hayo Ijumaa kwenye mkutano wa uchumi wa G-20 huko Pittsburgh, katika jimbo la Pennsylvania nchini Marekani.

Viongozi hao waliishutumu serikali ya Iran kwa kujenga mtambo wa siri wa kuzalisha mafuta ya nyuklia. Walisisitiza Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomi-IAEA, lipate fursa ya haraka kuhakikisha mtambo huo haujengwi ili kutengeneza silaha za nyuklia.

Maafisa wa utawala wa Obama wanasema ujenzi wa mtambo huo unakiuka maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linalotaka Iran kuacha urutubishaji wa madini ya uranium. Maafisa wa Iran wanasema shutuma za kuwepo mtambo wa siri ni za uongo. Mkuu wa nyuklia wa Iran, Ali Akbar Salehi, amesema shughuli za mtambo huo zipo ndani ya makubaliano ya mkataba wa IAEA.

XS
SM
MD
LG