Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 17:18

Kenya yaiachia ICC kufanya kazi yake


Kenya inasema mahakama ya kimataifa ya uhalifu-ICC, ipo huru kuwashtaki waliopanga njama za mauaji kwenye ghasia za baada ya uchaguzi mkuu nchini humo mwaka 2007.

Akizungumza katika mji wa Naivasha Jumatatu jioni, waziri wa sheria Mutula Kilonzo alisema Kenya haiwezi kufikia matakwa ya ICC yanayowataka kuunda mahakama ya ndani kwa watuhumiwa wa ghasia za uchaguzi ifikapo September 30. Kilonzo alisema mwendesha mashtaka mkuu wa ICC, Luis Moreno-Ocampo anaweza kushughulikia suala hilo.

Mwezi Julai, katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan alimpatia Moreno-Ocampo, orodha ya washukiwa katika ghasia za mwaka 2008. Watu 1,300 waliuwawa katika mapigano na mashambulizi yaliyozuka kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu wa urais nchini humo.

Bwana Annan alichangia kuwepo mkataba wa kushirikiana madaraka, ambao ulitatua mzozo wa uchaguzi na kupelekea kuundwa kwa serikali ya mseto ya Kenya.
Sauti ya Amerika imetembelea maeneo ya wakimbizi wa ndani ambao wanataka hatua za haraka zichukuliwe dhidi ya washukiwa hao.

XS
SM
MD
LG