Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 09:45

Obama awahimiza wabunge kufanya mageuzi ya huduma za afya


Rais wa Marekani Barack Obama aliliambia bunge la Marekani Jumatano usiku kuwa serikali kushindwa kushughulikia mageuzi ya huduma za afya kumewaacha wananchi bila ya bima wakiwa katika hatari ya kufilisika kama wakipata ajali moja au ugonjwa.

Bwana Obama alitoa maelezo ya mpango wake wa dola bilioni 900, ambao utajumuisha bima zinazoendeshwa na serikali ili kutoa ushindani kwa makampuni binafsi. Alisema mpango huo hautaongeza kiwango cha nakisi ya bajeti ya marekani, lakini utalipiwa kuondoa matumizi yasiyofaa katika mfumo wa sasa wa huduma za afya.

XS
SM
MD
LG