Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 23:00

Vyama vya upinzani Burundi vyalalamikia Chama Tawala


Na Mwandishi wetu Esther Githui-Ewart

Vyama vya upinzani nchini Burundi vimeanza kujiandaa kwa uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka ujao, huku vikishutumu chama tawala kwa kuchangia hali duni ya maisha nchini humo.

Wakati huo huo katibu mkuu wa chama tawala cha CNDD-FDD, amesema hana imani na tume iliyochaguliwa hivi karibuni kusimamia uchaguzi mkuu wa mwaka 2010. Kauli ya katibu mkuu huyo imezusha utata kwani chama tawala kilikabiliwa na shinikizo kubwa kutangaza utaratibu wa kuteua tume ya kusimamia uchaguzi.

Sauti ya Amerika imezungumza na msemaji wa chama cha upinzani cha FRODEBU, Pancras Shimpaye ambaye amesema kwa kweli wameshangaa kusikia tamko hilo kwa kuwa tume yenyewe ya uchaguzi haijaanza kazi rasmi, kwa kuwa haijapata vifaa, haijapewa pesa, haijapata sheria ya uchaguzi ili ianze mchakato wa kuanzisha kazi kamili ya uchaguzi na wangependa kujua ni kitu gani hasa kinaendelea kwenye tume ya uchaguzi, ni ugomvi gani uko kati ya tume ya uchaguzi na chama tawala, huwenda wameshawaambia kwamba tume ya uchaguzi haita mpendelea mtu yeyote, haita muibia mtu yeyote na haita msaidia mtu yeyote, wao watafuata sheria pekee.

XS
SM
MD
LG