Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 17:46

Wakenya wapinga uteuzi wa Jaji Ringera.


Bodi ya ushauri ya kupambana na ufisadi nchini Kenya-KACC, imepinga vikali uteuzi wa Jaji Aaron Ringera, kama mkurugenzi mkuu wa tume hiyo, kwa muda wa miaka mitano mingine.

Uteuzi huo uliofanywa na Rais Mwai Kibaki wa Kenya umezusha lawama kali kutoka kwa wanasheria na makundi yasiyo ya kiserikali nchini humo. Makundi hayo yanadai uamuzi wa Rais Kibaki kumrejesha tena Jaji Ringera kwenye wadhifa huo unakiuka sheria.

Mwenyekiti wa bodi ya ushauri kwenye tume hiyo bwana Okongo Omogen, ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha wanasheria nchini Kenya, anasema Rais Kibaki amekiuka sheria kuhusu uteuzi wa wakurugenzi wa tume hiyo na manaibu wao.

Wakati huo huo Sauti ya Amerika imezungumza na mwanasheria na mbunge wa zamani wa eneo la Kabate bwana Paul Muite, na kwanza kutaka kujua nini kilichopelekea bodi hiyo kupinga uteuzi wa Jaji Ringera.

XS
SM
MD
LG