Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 09:23

Hali Iran haitabiriki kwa sasa


Rais wa Marekani Barack Obama amekariri wasiwasi wake juu ya matukio nchini Iran kufuatia matokeo ya uchaguzi wa rais yaliyozusha ubishi na kusababisha maandamano katika mitaa na barabara za mji mkuu Tehran.

Akizungumza na sauti ya Amerika Jumatatu mchambuzi wa maswala ya kisiasa Profesa Xavery Lwaitama alisema maandamano yanayoonekana Tehran yanatokana na vijana na watu wanaotaka mabadiliko.

Alisema waandamanaji hao wangependa kuwa huru kutumia vyombo vya habari vya kisasa. Profesa Lwaitama alisema taifa la Iran limejikita katika misingi ya kidini na kwamba ushawishi wa nchi za magharibi huenda umechochea azma ya kuyataka mabadiliko.

Akizungumza kuhusu rais Mahmoud Ahmadinejad aliyechaguliwa kwa muhula wa pili, mhadhiri huyo wa chuo kikuu cha Dar-es-Salaam Tanzania, alielezea kuwa rais Ahmadinejad ana uungaji mkono wa viongozi wa wengi wa kidini akiwemo Ayatollah Ali Khamenei na kwamba anajionyesha kuwa mtu wa kawaida.

Profesa Lwaitama alisema huenda mpinzani wake Mir Hossein Mousavi amepigwa na mshangao sasa kwamba amewasha moto wa kisiasa asioweza kuzima kwa kupinga matokeo ya uchaguzi huo, na kwamba litakaloibuka baada ya ghasia hizi haliwezi kutabiriwa.

XS
SM
MD
LG