Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 12:47

Hasheem aingia NBA Draft


Hasheem Thabit mchezaji wa mpira wa kikapu wa Chuo Kikuu cha Connecticut (UConn) hapa Marekani atakuwa mchezaji wa kwanza kutoka nchini Tanzania kucheza mpira wa kikapu wa kulipwa hapa Marekani. Hasheem alitangaza uamuzi huo wa kuacha mwaka wake wa mwisho chuoni hapo na kujiunga na NBA baada ya kushauriana na familia yake na rafiki zake pamoja na kocha wake Jim Calhoun. Kocha huyo alipoulizwa alisema Hasheem yuko tayari kucheza katika ligi ya NBA ambayo hujulikana kwa mikiki mizito na yenye upinzani wa hali ya juu kocha huyo aliongeza kuwa Hasheem ni mmoja wa wachezaji wakali katika difensi kwenye historia ya mpira wa kikapu wa vyuo na pia atakumbukwa kama mmoja wa wachezaji wazuri katika historia ya Uconn. Wachambuzi wa masuala ya michezo wanasema timu kama za Oklahoma City Thunder na Sacramento Kings zinahitaji wachezaji wa kati na wenye uwezo kwani Hasheem ameonyesha uwezo mkubwa katika Ulinzi na kuchaguliwa mchezaji bora wa mwaka kwa hivyo timu hizo zitakuwa zikimwangalia kwa makini.Naye Hasheem Thabit atakuwa kati ya wachezaji watano wa juu wa kwanza watakaochaguliwa. Timu hizo za NBA ambazo hupendelea zaidi wachezaji warefu hufanya uchaguzi wao wa wachezaji mwezi Juni kila mwaka na wachezaji wanaochaguliwa katika raundi ya kwanza hulipwa kima cha chini dola milioni tatu kwa mwaka.Hasheem Thabit anafit vizuri kwenye timu hizi kwani urefu wake ni futi 7.3. Hasheem ameweka rekodi ya pointi 13.6 rebound 10.8 na kuzuia au blocks 4.2 kwa mchezo na kuisaidia timu yake ya Huskies kwenda kwenye nusu fainali za vyuo maarufu kama "Final Four" mwezi uliopita. Chuo hicho kimesema Hasheem anapanga kuchukua ajenti kitendo ambacho kinaondoa uwezekano wa yeye kujitoa kwenye kinyang'anyiro hicho kabla ya Juni 15 na kurudi chuoni.

XS
SM
MD
LG