Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 23:42

Haki za Binadamu Zaendelea Kukiukwa Burundi


Shirika la kutetea haki za binadamu nchini Burundi, ITEKA limetoa ripoti na kusema licha ya mafanikio ya kisiasa yaliyofikiwa nchini humo, bado hali ya kisiasa haijawa bora zaidi ikilinganishwa na miaka michache iliyopita.

Mwenyekiti wa shirika la kutetea haki za binadamu nchini Burundi, David Nahimana, hali ya kibinadamu nchini Burundi kwa mwaka 2088 bado ni mbaya ikilinganishwa na mwaka mmoja uliotangulia.

Ripoti ya shirika hilo inasema watu 614 waliuawa, idadi ambayo ni chini kidogo ya watu 641 waliouawa mwaka mmoja kabla. Aidha inasema wanawake 998 walibakwa katika sehemu mbalimbali za nchi hiyo, hususani katika mikoa ya Bubanza na Bujumbura vijijini magharibi mwa Burundi.

Linasema waliohusika na vitendo hivyo ni waasi wa FNL, baadhi ya wanajeshi wa serikali na raia wa kawaida ambao bado hawajulikani. .

XS
SM
MD
LG