Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 09:11

Kibaki, Odinga Kuwafukuza Wala Rushwa


Kufuatia shinikizo kutoka wananchi, viongozi wa kidini na wanadiplomasia kutoka nchi za nje, Rais Mwai Kibaki na Waziri Mkuu Raila Odinga wanasema wako tayari kuwafukuza kazi mawaziri wanao jihusisha na rushwa.

Denis Onyango, msemaji wa waziri mkuu wa Kenya ameiambia Sauti ya Amerika kuwa Bwana Odinga amekubaliana na Rais Kibaki kuwa uchunguzi utafanyika, na kwamba yeyote atakaye patikana na hatia ya kujihusisha na rushwa ataachishwa kazi.

Onyango amesema watu watakuwa na uwezo wa kuwashinikiza viongozi wanaodhaniwa kujihusisha na rushwa au vitendo vingine viovu wajihuzulu, ili kuruhusu uchunguzi ufanyike.

Akiongea kuhusu kashfa ya mahindi, Onyango alisema mwanzoni kulikuwa na mvutano kati ya watu waliotaka waziri wa kilimo ajihuzulu, kwa maelezo kuwa alishindwa kudhibiti tatizo hilo, na wale waliotaka uchunguzi ufanyike kwanza kabla ya kuchukua hatua kama hiyo.

Lakini Onyango anasema kwa sasa kuna makubaliano kuwa yeyote anayedhaniwa kuhusika na rushwa itabidi aachie madaraka kwanza kuruhusu uchunguzi ufanyike.

Zinazohusiana

XS
SM
MD
LG