Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 16:22

ICC: Bashir Akamatwe


Mahakama hiyo yenye makao yake The Hague, ilitoa hati hiyo ya kukamatwa Rais Bashir Jumatano, baada ya jopo la majaji watatu kutumia miezi kadhaa kutafakari suala hilo. Majaji hao wanasema kuna ushahidi kuwa Bwana Bashir alisimamia kampeni ya mashambulizi dhidi ya raia wa Darfur, ambapo serikali yake imekuwa ikipambana na waasi tangu 2003.

Maoni ya awali kuhusu uamuzi huo wa mahakama yamekuwa mchanganyiko, huku makundi ya kutetea haki za binadamu yakipongeza uamuzi huo, na watu wanao-unga mkono Sudan wakisema ni uamzi wa hatari.

Profesa Xavier Lwaitama wa chuo kikuu cha Dar es Salaam ambaye awali alikuwa na mashaka kuhusu uamuzi kama huo, amesema kuna haja ya nchi zote za Afrika kushirikiana na mahakama hayo. hapo awali Profesa Lwaitama alikua na msimamo kuwa huenda hatua kama hiyo inaweza kusababisha machafuko zaidi.

Mashirika ya kutetea haki za binadamu, Amnesty International na Human Rights Watch, wanasema kuwa uamzi huo wa mahakama ya kimataifa ni ishara muhimu kuwa hata watu wenye nguvu wanaweza kuwajibishwa kwa uhalifu wa kivita.

Save Darfur Coalition wanasema hati hiyo inaongeza msukumo dhidi ya Rais Bashir, na kwamba inatoa mwanya wa kujadili suala la amani Darfur.

XS
SM
MD
LG