Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 14:58

Clinton Ziarani Asia


Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton anaendelea na ziara yake ya bara Asia leo akiwa amewasili Korea Kusini. Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwasili Seoul waziri Clinton alieleza wasiwasi wake kuhusu uongozi wa Korea Kaskazini na mgogoro unaoweza kutokea Kim Jong Il akiondoka madarakani.

Clinton alisema serikali ya Marekani ina wasiwasi sana kuhusu mabadiliko ya uongozi Pyongyang na uwezekano wake wa kuvuruga hali ya kisiasa katika eneo hilo la Asia.

Mwanadiplomasia huyo wa juu wa Marekani tayari ametembelea Japan naIndonesia. Ataelekea China kutoka Korea Kusin. Anasema ziara yake nchi za nje inakusudia kuonyesha kuwa uhusiano kati ya Washington na Asia-Pacific ni muhimu katika kuelezea changamoto zinazoikabili dunia.

Zinazohusiana

XS
SM
MD
LG