Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 08:58

Walinda Amani Washindwa Kuwalinda Raia DRC


Shirika la madaktari wasio na mipaka (Doctors without Borders) linasema walinda amani wa Umoja wa Mataifa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, hawafanyi juhudi za kutosha kuwalinda raia dhidi ya mashambulizi ya waasi wa Lord's Resistance Army (LRA).

Tangu Disemba mwaka uliopita, wakati serikali za Uganda, DRC na Sudan Kusini zilipoanzisha oparesheni ya kijeshi mashariki mwa Congo dhidi ya LRA, waasi wameuwa zaidi ya raia 900 kulipiza kisasi.

Madaktari wasio na mipaka wanasema mashambulizi hayo ya waasi yamekuwa ya kikatili, wanaume, wanawake na watoto wamekuwa wakiuwawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali hadi kufa au kutundikwa kwenye mti kama mshikaki wakiwa hai.

Shirika hilo la madaktari linasema wanajeshi wa kulinda amani 100 wa MONUC waliopo katika eneo hilo, wameshindwa kuwalinda raia, badala yake wanajishughulisha zaidi kutoa ushauri wa kitaalamu kwa kwa jeshi la serikali ya Congo.


Zinazohusiana

XS
SM
MD
LG