Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 02:40

Lubanga Akana Mashitaka ya Uhalifu wa Kivita


Mbabe wa zamani wa kivita nchini DRC Thomas Lubanga ameiambia mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita kuwa hana hatia ya mashitaka yanayo mkabili, ambayo ni kuwaingiza watoto katika jeshi na kuwapeleka uwanja wa vita.

Lubanga na kundi lake wanashutumiwa kuandikisha na kuwafundisha mamia ya watoto kuuwa, kutesa na kubaka wanawake mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika kipindi cha mwaka 2002 na 2003.

Lakini alipoulizwa Jumatatu na Jaji, Sir Adrian Fulford wa mahakama ya kimataifa ICC, Lubanga alikana mashitaka hayo kupitia mwanasheria wake. Dazeni kadhaa za mashahidi wanatazamiwa kutoa ushahidi wao mahakamani hapo katika kesi ambayo ni yakwanza kusikilizwa na hakama hiyo ya uhalifu wa kivita tangu ilipoanzishwa mwaka 2002.

Mwendesha mashitaka mkuu Luis Moreno-Ocampo aliiambia mahakama kuwa baadhi ya watoto wanajeshi waliopewa mafunzo na kundi la Lubanga, sasa wanatumia madawa ya kulevya na wengine wanajihusisha na ukahaba.

Zinazohusiana

XS
SM
MD
LG