Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 05:13

Burundi: Afisi za CNDD/FDD zatiwa moto


Chama tawala cha CNDD FDD huko Burundi kinakanusha kuhusika kwa wanachama wake katika kutia moto karibu afisi zake 15 kote nchini. Msemaji wa chama Gerald Daniel Ndabirabe, anasema wanasubiri uchunguzi wa maafisa wa usalama kuweza kujua walohusika na kutoa mwito kwa raia kutoingilia kati mzozo huo.

Akizungumza na sauti ya amerika Bw Ndabirabe alisema hawezi kujua au kulaumu chama chechote kabla ya matokeo ya uchunguzi wa usalama kukamilika. Hata hivyo amelani vikali vitendo hivyo

Kwa upande wake chama kidogo cha upinzani cha UPD kimekanusha katu kuhusika kikidai kwamba vijikaratasi vimetawanywa na walohusika na inavyo onekana ni wanachama wa chama tawala.

Katibu mkuu wa chama cha UPD, Cheauvineau Mbwengezo, akizungumza na Sauti ya Amerika anasema vitendo hivyo vinakwenda kinyume na misingi ya kidemokrasia na kwamba chama chao kinahamasisha zaidi kulinda taasisi za kidemokrasia kwa faida ya nchi na hatua walofika hadi hii leo.

Mbwengezo anasisitiza kwamba mvutano unaoendelea ndani ya chama cha CNDD FDD kimesababisha baadhi ya wanachama wake kukihama na hivyo kusababisha wasi wasi miongoni mwa viongozi wao. Matokeo yake anasema wanachama wa UPD wamekua wakikamatwa na chama kunyanyaswa.

Kufuatana na redio ya taifa miongoni mwa afisi zilizotiwa moto zilikua katika majimbo ya Bubanza, Cibitoke, Ngozi, Kayanza na Karuzi.


XS
SM
MD
LG