Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 01:41

Kenya Yatoa Onyo kwa Rais wa Somalia


Serikali ya Kenya imetoa onyo kali kwa Rais Abdullahi Yusuf wa Somalia kufuatia hatua yake ya kumfuta kazi Waziri Mkuu Nur Hassan Hussein, kwa maelezo kuwa hatua hiyo inazuwia kurejea kwa amani na maridhiano nchini Somalia.

Waziri wa mambo ya nje wa Kenya Moses Wetangula amesema kuwa Rais Abdullahi Yusuf amefanya makosa kumfukuza kazi Waziri Mkuu Nur Hassan Hussein baada ya viongozi hao wawili kushindwa kukubaliana kuhusu muundo wa baraza la mawaziri.

Kwa mujibu wa bwana Wetangula, serikali ya Kenya itawawekea vikwazo vya fedha na kuwazuwia kuingia Kenya viongozi wa Somalia,ndugu na marafiki zao wanaokwamisha juhudi za kuleta amani nchini Somalia.

Bwana Wetangula ameweka wazi kuwa uamuzi huo unatokana na hatua ya rais Yusuf kumfukuza kazi Waziri Mkuu Nur Hassan Hussein. Anasema, "Waziri mkuu amekwenda Baidoa, bunge limesema linaimani naye, waziri mkuu ameteuwa baraza la mawaziri, bunge limeiidhinisha na kukubali, rais ameteuwa mtu mwingine na kusema huyo ndiye atakuwa waziri mkuu."

Waziri Mkuu Nur Hassan Hussein aliteuliwa na Rais Abdullahi Yusuf baada ya kujiuzulu kwa waziri mkuu wa zamani Ali Mohamed Guled.

XS
SM
MD
LG