Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 16:49

Watu Wenye Silaha Wapora Mali DRC


Wafanya biashara mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanasema jana watu wenye silaha walipora mali katika miji ya Kanyabayonga, Kirumba na Kayna na kuongeza hali ya wasiwasi kwa wananchi ambao tayari wanakabiliwa na hali mbaya ya mapigano kati ya majeshi ya serikali na waasi wanaoongozwa na Jenerali Laurent Nkunda.

Kiongozi wa wafanya biashara, Policarpe Ndivito ameiambia Sauti ya Amerika kuwa watu hao waliokuwa wamevaa nguo za kijeshi walipiga risasi huku na huko wakati wakibomoa na kupora mali ndani ya maduka.

Kwa mujibu wa Ndivito wakazi wa miji hiyo iliyopo kilomita 180 kaskazini mwa mji wa Goma wamelazimika kuyahama makazi yao kwa kuhofia usalama wao. Haikuweza kufahamika mara moja kama kuna watu waliouwawa au kujeruhiwa.

Bwana Ndivito anasema hali ya maisha ni mbaya mno mashariki mwa DRC kufuatia mapigano yanayo endelea kati ya waasi wa CNDP na majeshi ya serikali, na kuomba jumuiya ya kimataifa, hususan mataifa jirani kusaidia juhudi za kuleta amani nchini humo.

XS
SM
MD
LG