Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 09:07

Obama Apata Ushindi wa Kihistoria


Mgombea urais wa chama cha Democratic Seneta Barack Obama, jana alipata ushindi mkubwa na kumshinda mpinzani wake wa chama cha Republican Seneta John McCain wa Arizona.

Ushindi wa Seneta Obama ulisherehekewa katika jimbo la Chicago, ambapo maelfu kwa maelfu ya watu walimiminika kutoka kila kona ya Marekani kushiriki katika tukio hilo la kihistoria.

Wengi wa watu hao walifunga safari kutoka maeneo ya mbali wakiwa na matumaini kuwa mgombea wao angeweza kuibuka mshindi.

Kwingineko nchini, watu walikaa karibu na televisheni zao wakiangalia wakati matokeo yalipokuwa yakitajwa kutoka kila jimbo.

Matumaini ya warepublican yalipotea baada ya kupoteza Pennyslivania na Ohio, majimbo ambayo walitakiwa kushinda kuingia White House.

Makao makuu ya republican hapa Washington DC na kwingineko nchini yalikuwa yamepoa wakati wa kipindi chote cha kusubiri matokeo.

Kwa upande mwingine wademocratic walikuwa na shamla shamla, vigeregere na nderemo baada ya kusikia kuwa jimbo la Ohio na Pennyslivania yameangukia mikononi mwao.

Baada ya taarifa kutolewa kuwa Seneta Obama alikuwa mshindi wa urais, watu walikumbatiana, na kuonyesha furaha ya kiwango cha juu--huku wengine wakiangua kilio cha furaha.

Akihutubia wafuasi wake waliokuwa wamesimama sehemu ya wazi, bwana Obama aliwashukuru wafuasi wake, na kueleza baadhi ya mabadiliko anayo tarajia kuyafanya wakati wa kipindi chake cha urais.

Obama alikuwa na ujumbe kwa wale ambao pengine walikuwa bado wana mashaka kuwa Marekani ni sehemu ambapo mambo yote yanawezekana. Alisema, "Wale ambao bado wana hoji nguvu ya demokrasia yetu, leo ni jibu lenu."

Baada ya kupata uhakika kuwa alikuwa ameshinda uchaguzi, mpinzani wake Seneta John McCain alisimama mbele ya taifa na kumpongeza Obama kufuatia ushindi wake.

Aidha Seneta McCain aliwaomba wafuasi wake kuweka tofauti zao na kumuunga mkono rais mteule, Barack Obama.

XS
SM
MD
LG