Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 23:15

Sakata la vyeti feki laibuliwa tena na Magufuli


Rais Magufuli
Rais Magufuli

Rais John Magufuli ametoa tamko kuhusu sakata la vyeti feki na kuwaambia wananchi kuwa "nasubiri kukamilika kwa ripoti ya uchunguzi huo ilinifanye maamuzi.

Rais alisema hayo jana mubashara katika mitandao ya jamii wakati akizindua majengo ya mabweni ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), yaliojengwa na Wakala wa Majengo (TBA) ambayo yatakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 3,840.

Sakata la vyeti vya kughushi limekuwa kubwa baada ya mmoja wa wateule wa Rais Magufuli, ambaye hivi sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kushutumiwa kuwa anatumia 'vyeti vya kughushi' baada ya kufeli elimu ya sekondari na kusababisha watu mbalimbali kumsihi mkuu huyo wa nchi atengue uteuzi wake.

Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wamezungumzia elimu ya mteule huyo kwenye vikao vya Bunge, wakitaka Rais atengue uteuzi wake, huku Meya wa Ubungo, Boniface Jacob akiliwasilisha suala hilo mbele ya Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Vyombo vya habari nchini Tanzania vimeripoti kuwa askofu Josephat Gwajima alisema kuwa ana ushahidi wa suala hilo, na pia msanii Nay alitoa wimbo wa “Wapo” unaosema mtu anayeitwa Daudi Bashite ndiye 'jipu jipya' nchini na kuhoji sababu za Rais Magufuli kutotengua uteuzi wake.

Baada ya kimya cha muda mrefu, Rais Magufuli alisema hivi karibuni katika hafla ya uzinduzi wa barabara za juu katika makutano ya Barabara ya Morogoro na Sam Nujoma, kuwa wananchi wasipoteze muda kuzungumzia mambo ya mitandaoni na kumtaka mteule huyo kuendelea “kuchapa kazi”.

Lakini jana, Rais aligusia kwa kifupi suala la kughushi vyeti wakati akizindua mabweni ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam sehemu ya Mlimani na kusema anasubiri ripoti ya uchunguzi huo iliafanye maamuzi.

XS
SM
MD
LG