Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 05:21

Wakenya wawika katika mbio za nyika Kampala

Timu ya Kenya ya mchanganyiko Asbel Kiprop, Beatrice Chepkoech, Winnie Mbithe and Bernard Koros
Timu ya Kenya ya mchanganyiko Asbel Kiprop, Beatrice Chepkoech, Winnie Mbithe and Bernard Koros

Wakiongozwa na Irene Chepet Cheptai, wanariadha wanawake wa Kenya walionyesha uhodari wa kipekee wa jinsi ya kushindana katika masafa marefu, na kuweka historia, walipochukua nafasi zote sita za juu katika mashindano ya ubingwa wa dunia wa mbio za nyika.

Irene Cheptai wa Kenya ashinda dhahabu mbiyo za wanyika Kampala Uganda 2017
Irene Cheptai wa Kenya ashinda dhahabu mbiyo za wanyika Kampala Uganda 2017

Cheptai aliyewasili Uganda mwishoni mwa wiki akiwa hajashindwa katika mbio za nyika mnamo msimu huu wote, aliwapita wenzake Alice Aprot na Lilian Kassait Rengeruk katika kilomita ya mwisho na kunyakua ushindi kwa kutumia dakika 31 sekunde 57 katika mbiyo hizo za kilomita 10.

Cheptai alisema baadae kwamba mashindano yalikua makali lakini ushindi wao unatokana na kushirikiana pamoja na kusaidiana.

Kwa upande wa wanaume, mkenya mwenzao Goffrey Kamworor alitetea ubingwa wake katika mbiyo za kilomita 12 alipomshinda mwenzake Leonard Barsoton aliyenyakua fedha na methopia Abadi Hadis kuchukua shaba.

Jacob Kiplimo ameipatia Uganda dhahabu yake pekee na ya kwanza aliposhinda za vijana chini ya miaka 20.

Jacob Kiplimo akishinda mbiyo za nyika za vijana chini ya miaka 20 Kampala
Jacob Kiplimo akishinda mbiyo za nyika za vijana chini ya miaka 20 Kampala

Wakikimbia kukiwa na joto kali huko Kampala, Gidey Letesenbet aliokowa Ethopia kwa kiunyakua dhahabu katika mbiyo za vijana chini ya miaka 20, akiwa mwanamke wa kwanza kushinda mara mbili mfululizo katika daraja yake.

Letesenbet Gidey wa Ethopia ashinda mbiyo za wanawake U20 mjini Kampala
Letesenbet Gidey wa Ethopia ashinda mbiyo za wanawake U20 mjini Kampala

XS
SM
MD
LG