Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 10:33

Marekani: Ndoto ya Wahamiaji Kutoka Afrika Itagonga Mwamba?


Takwimu za wahamiaji Marekani waliotokea Afrika
Takwimu za wahamiaji Marekani waliotokea Afrika

Marekani inaendelea kuwa ni kivutio cha wahamiaji kutoka Afrika, idadi yao ikiongezeka maradufu tangu mwaka 2000.

Ingawaje wengi wao wanatokea nchi zilizoathiriwa na vita, bado idadi kubwa ya wahamiaji hao ni wenye weledi na walioelimika.

Kwa mujibu wa tafiti za Kituo cha Utafiti cha Pew, mwaka 2015, kulikuwa na takriban watu milioni 2.1 waliokuwa wakiishi Marekani wenye asili ya Kiafrika. Idadi hiyo imeongezeka kutoka 880,000 mwaka 2000 na 80,000 tu mwaka 1970.

Monica Anderson, mtafiti na mwandishi wa repoti hiyo, amesema namba hizo zinaongezeka maradufu takriban katika kila muongo na anaona kuwa mwelekeo huo utaendelea.

“Mwaka 1980 peke yake asilimia 1 ya wakimbizi walioruhusiwa kuingia Marekani walikuwa wanatokea Afrika, ambao leo hii idadi yao imefikia asilimia 37. Hiyo ni sababu moja kubwa inayopelekea kuongezeka kwa wahamiaji kutoka Afrika lakini haielezei habari nzima juu ya uhamiaji,” mtafiti huyo ameiambia VOA.

Anderson anasema kuwa vikundi mbalimbali vya wahamiaji mahiri wamebadilisha maeneo kama Minnesota ambayo ni makazi ya watu 25,000 wenye asili ya Kisomali, ambayo ni takriban moja ya tano ya wahamiaji waliozaliwa Marekani.

Wanigeria ndio wenye idadi kubwa ya diaspora Marekani wakiwa 327,000, wakifuatiwa na Waethopia ambao ni 220,000 na Wamisri wao ni 192,000, Pew iligundua hilo katika utafiti wake. Majimbo ambayo wahamiaji wa kiafrika wanapendelea kwenda kuliko yote ni Texas, New York, California na Maryland.

Mengi ya majimbo haya Marekani yana …idadi kubwa ya wahamiaji wa Kiafrika hivi sasa kuliko ilivyokuwa siku za nyuma,” amesema Anderson. Katika makundi mbalimbali Marekani, Wahamiaji wa Kiafrika wanabadilisha idadi ya wahamiaji katika maeneo hayo.”

Hakuna anaejua vipi mabadiliko ya sera za uhamiaji yanaweza kuathiri wahamiaji kutoka Afrika.

Hivi karibuni wahamiaji wengi walishtushwa na amri ya kiutendaji ilisainiwa na Rais Donald Trump ikikataza wahamiaji kutoka nchi tatu za Kiafrika na kusimamisha programu ya Marekani ya kuwapa makazi wakimbizi.

Amri hiyo ilisitishwa na Mahakama ya Rufaa, lakini uongozi wa Trump umeahidi kurudisha tena.

Pendekezo jingine lilotolewa na Seneta Tom Cotton wa Republikan limetaka kupunguzwa kwa green cards zinazotolewa na Marekani, idadi ikiwa ni kati ya laki tano mpaka milioni moja.

“Ninavyoona ni suala lenye muendelezo iwapo wanafunzi wachache watakuja Marekani, au itakuwa vigumu sana watu kuwadhamini ndugu zao kuingia nchini.

Nafikiri ni mapema mno kujua iwapo hilo litatokea katika utawala wa Trump,” amesema Capps.

Lakini kama hakuna mabadiliko makubwa, wahamiaji wa Kiafrika wanatarajiwa kuendelea kuongezeka ilivyokuwa kwamba uchumi wa Marekani unaendelea kuwa imara ukitoa fursa kwa wahamiaji.

Marekani ina soko kubwa la ajira, ambalo ni soko lenye nguvu katika ajira,” amesema Capps.

“Ni soko kubwa sana la ajira ukilinganisha na nchi nyingine nyingi ambazo wahamiaji wakiafrika pengine wangetaka kwenda huko na wengi wa wahamiaji hapa Marekani wana mafanikio mazuri. Kwa hiyo nafikiri kama hakutokuwa na masharti ya ziada, mabadiliko makubwa ya sera ya uhamiaji Marekani, bado kutakuwa na vivutio venye nguvu vya kuwafanya watu waje Marekani.”

XS
SM
MD
LG