Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 10:40

White House: Trump Alimlazimisha Flynn Kujiuzulu


Rais Donald Trump
Rais Donald Trump

Rais wa Marekani Donald Trump alimlazimisha aliyekuwa Mshauri wa Usalama wa Taifa Michael Flynn kujiuzulu kwa sababu ya kuendelea kuona "uaminifu wake unatetereka" na kufuatia maelezo yake kuhusu uhusiano wake na Russia, White House imesema Jumanne.

Msemaji wa White House Sean Spicer amesema, "Rais amesema hana imani tena na mshauri wa usalama wa taifa."

Flynn jenerali mstaafu wa jeshi, aliondolewa madarakani Jumatatu usiku baada ya kuwa ni mshauri muhimu wa juu wa Trump kwa wiki tatu, kitu ambacho ni nadra kutokea kwa kiongozi wa ngazi ya juu wakati rais ndio kwanza kachukua madaraka.

Spicer amesema Trump amefurahi kuwa Flynn alikuwa amezungumza na Sergey Kislyak, balozi wa Russia nchini Marekani, na kuhitimisha kuwa hakukuwa na uvunjaji sheria wowote katika mazungumzo yao, na kuwa Flynn wakati huo alikuwa ni raia wa kawaida, sio afisa wa serikali.

Jenerali mstaafu Michael Flynn, alijiuzulu kufuatia kashfa iliyomkumba kuhusiana na mazungumzo aliyofanya na balozi wa Russia nchini Marekani, Sergey Kislyak, ambayo yalikuwa yamezua utata na mjadala mkubwa Marekani.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Associated Press, Flynn, aliwasilisha barua ya kujiuzulu kwa rais Donald Trump Jumatatu usiku.

Katika barua yake Flynn amesema alifanya mawasiliano kadhaa na balozi wa Russia wakati wa kipindi cha mpito, na kumpa Makamu wa Rais, Mike Pence "habari ambazo hazikukamilika."

XS
SM
MD
LG