Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 16:59

Museveni afanya mabadiliko makubwa katika jeshi


Makamanda wa Kikosi maalum cha Uganda wakati wa zowezi la kushtukiza
Makamanda wa Kikosi maalum cha Uganda wakati wa zowezi la kushtukiza

Rais wa Uganda Yoweri Museveni Jumatatu usiku amefanya mabadiliko makubwa katika jeshi la Uganda na baraza lake la mawaziri na kumondowa mkuu wa majeshi Jenerali Katumba Wamala.

Katika mabadiliko hayo nafasi ya Jenerali Wamala imechukuliwa na Meja Jenerali David Muhoozi ambae kabla ya uteuzi huu alikuwa mkuu wa jeshi la nchi kavu.

Msemaji wa UPDF Luteni Kanali Paddy Ankunda amethibitisha mabadiliko hayo, lakini alipoulizwa Jumanne asubuhi kuhusu mabadiliko haya alisema hakuwa na taarifa zozote.na anataraji kutoa taarifa kamili baadaye Jumanne.

Kadhalika Brigedia Peter Elwelu, alikyeongoza mashambulizi dhidi ya Kasri ya mfalme wa Rwenzururu ambayo yalisababisha vifo vya watu 100 mwezi wa Disemba, amepandishwa cheo na kuwa Meja Jenerali na kupewa jukumu la kuongoza jeshi la nchi kavu.

Jenerali Katumba Wamala mkuu wa majeshi ya Uganda
Jenerali Katumba Wamala mkuu wa majeshi ya Uganda

Jenerali Katumba Wamala ambaye alikuwa mkuu wa majeshi amechaguliwa kuwa waziri katika ofisi ya rais anaye shughulikia masuala ya ujenzi mara baada ya kupitishwa na bunge ataanza kazi mara moja.

Wakati huo huo Rais Museveni amemuodosha mtoto wake Meja Generali Muhoozi Kainerugaba kutoka nafasi ya mkuu wa kikosi maalumu (SFC) na kumchagua kuwa mshauri maalumu wa rais katika masuala ya kila siku.

Nafasi ya mtoto wa rais imechukuliwa na Luteni Kanali Don Nabaasa aliyepandishwa cheo kuwa Kanali na atakaimu kikosi cha SFC.

Meja Jenerali Muhoozi Kainerugaba, mkuu wa kikosi maalum SFC
Meja Jenerali Muhoozi Kainerugaba, mkuu wa kikosi maalum SFC

Meja Jenerali Mbadi ambaye alikuwa ndio mndhimu wa jeshi sasa ni naibu mkuu wa majeshi. Kwa muda mrefu Meja Jenerali Mbadi alikuwa ni mlinzi wa rais Museveni.

Nae Luteni Jenerali Charles Angina ambaye alikuwa naibu wa Jenerali Katumba ameondolewa na kupewa wadhifa wa naibu msimamizi wa operesheni za kubuni rasilmali.

XS
SM
MD
LG