Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 11:44

Kenyatta atoa pendekezo kwa madaktari wanaogoma Kenya


Ouma Oluga, Katibu Mkuu wa chama cha madaktari Kenya (KMPDU), akiwahutubia madaktari wanaogoma.
Ouma Oluga, Katibu Mkuu wa chama cha madaktari Kenya (KMPDU), akiwahutubia madaktari wanaogoma.

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya hatimae amekutana na wawakilishi wa Chama cha Madaktari (KMPDU) katika Ikulu ya Mombasa siku ya Juamtano katika juhudi za kuwataka wamalize mgomo wao unaoendelea kwa zaidi ya mwezi moja sasa.

Taarifa ya Ikulu inaeleza kwamba Rais Kenyatta aliwasilisha pendekezo kwa ujumbe wa madaktari ikiwa ni pamoja na kukubali kuongeza mishahara ya madaktari kwa asili mia 100 katika takriban viwango vyote.

Ujumbe wa KMPDU ukiongozwa na mwenyekiti wake Dr Samuel Oroko, umeeleza nia ya madaktari kurudi kazini ikiwa madai yao ya nyongeza za mishahara na marupurupu yatakubaliwa.

Hata hivyo ujumbe huo umeomba muda ili kuweza kushauriana na wanachama wao juu ya pendekezo hilo jipya kabla ya kuchukua uwamuzi.

Aidha madaktari walidai nyongeza za mishahara ya hadi asili mia 300, na kulipwa mishahara ya miezi ya nyuma pamoja na kuhakikishiwa mazingira bora ya kazi kabla ya kurudi kazini.

Taarifa ya ikulu inaeleza kwamba katika juhudi za kuimarisha mazingira ya kazi ya madaktari, serikali imetoa pendekezo jipya la kuwepo posho ya dharura ya kiasi KSh 10,000 kwa mwezi.

Wachambuzi wanasema mkutano huo ni ishara kwamba serikali hivi sasa imetambua madai ya madaktari na wauguzi na kuna matumaini tatizo hilo litapatiwa ufumbuzi wa haraka.

XS
SM
MD
LG