Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 21:35

Ethopia yatangaza utawala wa dharura


Ethiopia yatangaza amri ya dharura
please wait

No media source currently available

0:00 0:02:29 0:00

Waziri mkuu wa Ethopia Hailemariam Desalegn, ametangaza miezi sita ya utawala wa dharura, akisema amri hiyo inalengo la kurudisha tena utulivu na utawala wa sheria baada ya wiki kadhaa ya maandamano na ghasia zilizosababisha vifo na uharibifu mkubwa wa mali.

Polisi wakifyetua mabomu ya machozi wakati wa sherehe za Irrecha
Polisi wakifyetua mabomu ya machozi wakati wa sherehe za Irrecha

Wiki hii waandamanaji wametia moto viwanda vinavyomilikiwa na wageni, shamba la maua na magari, na kusababisha hasara kubwa ya kiuchumi na idadi ya walofariki kuongezeka kutokana na malalamiko dhidi ya haki za kiraia na kunyakuliwa kwa ardhi na serikali.

Akihutubia taifa kupitia televisheni ya taifa siku ya Jumapili Hailemariam amesema “hali ya dharura imetangazwa kwa sababu hali imekua tishio kwa wananchi wa taifa hili. Hali ya dharura ni muhimu katika kudumisha tena Amani na uthabati katika kipindi kifupi.”

Waziri mkuu alisema muungano unaotawala waEPDRF, utatafakarti pia juu ya mageuzi na kupanga kuanza mazungumzo na upinzani.

Ghasia hizo zimeweka dosar kubwa katika taifa ambako ukuwaji wa viwanda ulongozwa na serikali umepelekea Ethopia kua moja wapo ya nchi yenye ukuwaji wa haraka wa uchumi barani Afrika, lakini mahala ambako serikali inazidi kukosolewa na jumuia ya kimataifa na upinzani wa umaa kutokana na muelekeo wake wa kimabavu katika maendeleo na utawala.

Reli mpya ya usafiri kati ya Ethopia na Djibuti yafunguliwa
Reli mpya ya usafiri kati ya Ethopia na Djibuti yafunguliwa

Siku ya Jumamosi tovuti ya seriukali imethibitisha kwamba makampuni 11 kuanzia kampuni za nguo hadi shamba la biashara ya mauwa yameshambuliwa na waandamanaji na kutiwa moto pamoja na magari 60.

Ghasia zimetokea nje ya mji mkuu wa Addis Ababa, na ni karibu wiki moja baada ya watu 55 kuuiwawa kwa kukanyagwa katika sherehe za kila mwaka kusini mashariki ya mji mkuu baada ya polisi kufyetua mabomu ya kutoa machozi kwa waandamanaji.

Ghasia zinatokana na juhudi za serikali kuleta maendeleo ya viwanda nchini humo.

XS
SM
MD
LG