Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 01:46

Bunge la Marekani kujadili kurejesha Wasudan Kusini nyumbani


FILE - Watoto wa KiSudan katika kambi ya Kakuma Kenya, April 24, 2000.
FILE - Watoto wa KiSudan katika kambi ya Kakuma Kenya, April 24, 2000.

Karibu watu 500 - wanawake na wanaume - ambao zamani walikuwa wakijulikana kama "watoto waliopotea" kutoka Sudan Kusini, huenda wakarudi nyumbani karibuni kutoka Marekani kujenga nchi yao endapo mswaada uliowasilishwa Congress wiki hii utapita.

Mswaada huo utalipia gharama za usafiri kwa watu hao ambao kwa sasa wanafanya kazi Marekani na wanataka kutumia ujuzi wao kujenga nchi yao.

Mmoja wa watu hao waliokuwa wakijulikana kama "lost boys" ni David Acouth, ambaye anafanya mazoezi ya kazi katika ofisi ya mbunge Mdemokrat Karen Bass wa California ambaye ni mmoja wa wabunge walioandika mswaada huo. Anasema wakimbizi wengi wa Sudan Kusini walioelimika Marekani wamepata mafunzo katika tiba, elimu au huduma za afya ambayo yanaweza kusaidia watu wa Sudan Kusini.

FILE - Abraham Akoi, kushoto, and Emanuel Solomon wakizungumzia maswala ya nyumbani kwao Sudan Kusini.
FILE - Abraham Akoi, kushoto, and Emanuel Solomon wakizungumzia maswala ya nyumbani kwao Sudan Kusini.

​"Hakuna hospitali za kutosha Sudan Kusini, na tuna Wasudan Kusini wengi ambayo wanafanya kazi hapa kama wauuguzi au madaktari," alisema Acouth. "Tutakachofanya ni kuwapa watu hawa fursa ya kwenda Sudan Kusini. Wanaweza kufundisha wengine kuwa wauguzi na madaktari wasaidizi, wakati huo huo wakitoa huduma za afya kwa wananchi."

Chanzo miaka ya 80

Kundi la watu waliokuja kujulikana kama "watoto wa Sudan waliopotea" lilianza katika miaka ya kati ya 1980, wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe Sudan, ambayo ilikuwa bado haijagawanyika kuwa nchi mbili. Zaidi ya watoto wa kiume 20,000 waliokoseshwa makazi au kupoteza wazazi wakati wa vita vya miaka 20 walivumilia magumu mengi wakisafiri kwa mguu kuelekea kambi za wakimbizi nchini Ethiopia na Kenya.

Marekani hatimaye ilichukua karibu vijana wa kiume 3,800 katika miezi minane ya kwanza ya mwaka 2001. Mpango huo ulisimamishwa baada ya shambulizi la kigaidi la Sept. 11, 2001 dhidi ya Marekani, na kuanzishwa tena 2004 pale maelfu ya Wasudan waliporuhusiwa kuingia Marekani. Wengine walipokelewa Canada na nchi za Ulaya.

Jina "lost boys" au vijana waliopotea lilianza kutumiwa na wafanyakazi wa misaada, na kufufuliwa upya baada ya Sudan Kusini kupata uhuru na raundi mpya ya mapigano kuanza tena nchini humo mwaka 2013.

Mswaada uliowasilishwa wiki hii katika Kamati ya Mambo ya Nje ya Baraza la Wawakilishi la bunge la Marekani unataka kuwagharamia Wasudan Kusini 500 kurudi nyumbani lakini idadi hiyo inaweza kuongezeka, alisema Acouth.

Misaada ya awali

Marekani imetumia karibu dolla billioni 1.7 katika misaada kwa Sudan Kusini, wakati na baada ya vita vya 2013 kuzuka, pale mtafaruku wa kwanza ulipoanza baina ya makundi ya Rais Salva kiir na makamu wake Riek Machar.

Na kwa vile mapigano yameendelea Sudan Kusini kwa zaidi ya mwaka mmoja baada ya makubaliano ya amani kutiwa saini, baadhi ya wabunge wa Marekani huenda wakasita kuunga mkono mpango huu mpya.

XS
SM
MD
LG