Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 13:34

Rio 2016 yafungwa rasmi


Waziri mkuu wa Japan, Shinzo Abe akiwa katika uwanja wa Maracana.
Waziri mkuu wa Japan, Shinzo Abe akiwa katika uwanja wa Maracana.

Mashindano ya 31 ya Olympic ya Rio 2016 yamefungwa rasmi jijini Rio de Janairo, Brazil, na kukabidhi mji wa Tokyo, Japan mashindano yajayo ya mwaka 2020.

Mashidano hayo yamemalizika kwa Marekani kuibuka mshindi wa jumla kwa kujikusanyia medali 121, ikifuatiwa na China yenye medali 70, huku Uingereza ikishika nafasi ya 3, kwa kuchukuwa medali 67.

Waziri mkuu wa Japan, Shinzo Abe alikuwepo katika uwanja wa Maracana ilipofanyika sherehe za kufungwa Olympic ya mwaka huu 2016.

Kuiwakilisha Marekani, mwanasarakasi Simone Biles ambaye ni mshindi wa medali za dhahabu 4 na shaba 1, alipewa heshma ya kushika bendera ya Marekani, ikiwa ni ishara ya kufungwa rasmi mashindano hayo yanayofanyika kila baada ya miaka minne.

Katika sherehe za kufunga mashindano hayo mkimbiaji wa Kenya, wa Marathoni Eliud Kipchoge, alikabidhiwa medali yake ya dhahabu na kupigiwa wimbo wa taifa akiwa na mshindi wa medali za fedha na shaba.

XS
SM
MD
LG