Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 17:09

Waingereza wajuta kujiondoa Umoja wa Ulaya


Bango jipya likionesha uhusiano kati ya Uingereza na Marekani baada ya waingereza kuamua kujiondoa kutoka EU huko New York
Bango jipya likionesha uhusiano kati ya Uingereza na Marekani baada ya waingereza kuamua kujiondoa kutoka EU huko New York

Waingereza milioni mbili wametia saini waraka kutaka uwamuzi wa kujiondowa kwa Uingereza kutoka Umoja wa Ulaya kutoidhinishwa kua sheria na bunge la nchi hiyo na hata kutaka kura mpya ya maoni kuitishwa.

Siku mbili baada ya waingireza kupiga kura ya maoni kuamua kuondoka kutoka EU, maoni yanaendelea kuvuma katika kile wachambuzi wameeleza tukio lililosababisha tetemeko la ardhi katika jukwa la kisiasa na kifedha.

Mitandao ya kijamii imejaa maoni yenye hasira na wakati huo wasi wasi juu ya athari za kura hiyo, kukiwepo na wimbi la wengi wakidai wamejuta kupiga kura hiyo na kuanzishwa neon la #regrexit, au #whathavedone, “tumefanya nini”.

Mawaziri wa mambo ya nje wa mataifa 6 waanzilishi wa EU, wakutana Berlin
Mawaziri wa mambo ya nje wa mataifa 6 waanzilishi wa EU, wakutana Berlin

Hayo yakiendelea mawaziri wa mambo ya nchi za nje wa matiafa 6 wanzilizi wa Umoja wa Ulaya, Ujerumani, Ufaransa,Utaliana, Ubelgiji, Luxemburg na Uholanziwamekua wakikutana Jumamosi huko Berlin kujadili atahri za kura ya maoni ya Brexit .

Viongozi wa EU wanaitaka Uingereza kuanza mara moja utaratibu wa kujiondoa huku wakitaka pia kuanzishwa majadiliao juu ya ushirikiano mpya kati yao.

Wasi wasi pia umejitokeza juu ya uwezekano wa mataifa mengine yanachama kutaka kujiondowa pia.Vyama vya mrengo mkali wa kulia katika baadhi ya nchi za EU vimeanza kutoa wito wa kuitishwa kura ya maoni ya kujiondowa kwa nchi zao.

Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron ataelekea Brussels Jumane kwa mazungumzo na viongoziwa EU ambao wamepanga kukutana Jumatano kwa yao yakwanza bila ya Uingereza.

XS
SM
MD
LG